
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Kipolisi Nyamwaga SP Fatma Mbwana katika uzinduzi wa tamasha la michezo lilolenga kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili kwa watoto na wanawake wilayani hapo.
Nao baadhi ya wananchi wanazungumzia Suala la elimu kuendelea kutolewa kwenye jamii ili kutokomeza vitendo vya ukatili ambavyo vinaonekana kushamiri kwa siku hizi za karibuni kote nchini.