Monday , 17th Oct , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametoa msaada  kwa ajili ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu mkoani Geita kwa lengo la kuwapunguzia majukumu watu wanaovisimamia vituo hivyo mkoani humo.

Akikabidhi kwa niaba ya Rais Samia, mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigelaamewaonya wasimamisi wa vituo hivyo watakaoacha kuwapa watoto misaada hiyo kukumbana na mkono wa Sheria .
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa huo Professa Godius Kahyarara ameeleza zawadi zilizoachwa na Rais Samia.

"Zawadi alizoziacha hizi hasa zinalenga watu wenye mahitaji maalum hasa watoto yatima katika vituo vyetu mbalimbali katika mkoa wetu lakini vilevile vituo vya Imani kwa maana madrasa na vituo vya dini, kwahiyo ntapitia haraka haraka vitu alivyoviacha, kwanza ametupatia zawadi kubwa ya Mashuka, mablanket, mataulo, kuna pampers kwa ajili ya watoto wadogo, kuna mafuta ya kujipaka, kuna dawa za mswaki, kuna miswaki, themosi chupa cha chai, kuna sukari kuna sahani, kuna vikombe, kuna vijiko, kuna Kalamu, kuna misala Ile kwa ajili ya ibada na tasbih, kuna juzuu, kuna sukari na mchele kama nilivyosema, kwahiyo kwa kifupi zoezi hili hapa ni uwakilishi tu lakini litaendelea katika mkoa mzima, kwahiyo leo tuna kituo kimoja tumekipata mchana huu kitakuja kuchukua sehemu ya zawadi tulizozipata kutoka kwa Rais alizoziacha", alisema Kahyarara. 

Baadhi ya wasimamizi wa vituo waliopokea msaada huo wamemshukuru Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

"Kwa mara ya kwanza tunamshukuru mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada aliouleta kwa ajili ya kuwahudumia watoto, Mungu akubariki sana Rais kwa moyo wa upendo na  ukarimu kwa kuwalea watoto hawa, ninakushukuru sana pamoja na viongozi wote ambao mmeshirikiana kuupa mchango huu, hata kwa kuja kuwatembelea watoto, tunamshukuru na mkuu wa mkoa, hayupo nyuma yupo pamoja nasi akiktutembelea na  kutupa msaada wa hapa na pale, Mungu awabariki sana viongozi wa chama cha serikali kilichopo madarakani", alisema Godfrey