Friday , 18th Nov , 2022

Equatorial Guinea  inajiandaa na uchaguzi mkuu wa Urais wakati ambapo kampeni zinatarajiwa kumalizika Ijumaa ya leo kwa ajili ya uchaguzi wa urais na wabunge nchini humo.

Rais Teodoro Obiang Nguema anawania muhula wake wa sita mfululizo madarakani.

Zaidi ya wapiga kura 300,000 wamesajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo wa Jumapili.

Viongozi wa upinzani Andrés Esono Ondo na Buenaventura Monsuy Asumu wanatarajiwa kupambana na rais wa muda mrefu Teodoro Obiang Nguema ambaye anawania muhula wake wa sita mfululizo madarakani.