
Wakizungumza na #EATV hii leo Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Yusuph Makamba Mahuvi Mapembe amesema kwa mwaka jana shule hiyo iliandikisha watoto 316 huku kwa mwaka huu mpaka sasa ni watoto 169 ambapo
akizungumza kwa niaba ya Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mpakani iliyopo kata ya mabibo mwenyakiti wa serikali ya mtaa wa jitegemee Yusuph Abdallah amesema shule hiyo Mpakani imeshaandikisha wanafunzi 100 mpaka sasa lakini lengo likiwa ni kufikia wanafunzi 200
Nao baadhi ya wazazi waliofika kuandikisha watoto wao kujiunga na darasa la kwanza wamesema katika uandikishaji wa watoto wao changamoto kubwa waliyokutana nayo ni kukosa vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao jambo lililowalazimu kuchelewa kumuandikisha mtoto wake
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Maguruwe Peter Siro iliyopo shule ya msingi Yusuph Makamba amesema wanaanza kupita nyumba Hadi nyumba kuwabaini wazazi ambao Wana watoto wenye umri wa kwenda shule lakini bado hawajawapelekakuwaandikisja Ili wawachukulie hatua za kisheria kama serikali ilivyowaelekeza