
Kiongozi wa huyo wa zamani alipatikana na hatia ya kuuza pasipoti kwa watu wasio na utaifa wanaoishi katika Ghuba na alikuwa ameshtakiwa kwa ubadhirifu wa mamilioni ya dola.
Akitolea mfano wa kesi isiyo ya haki, Sambi mwenye umri wa miaka 64, alikataa kuhudhuria vikao hivyo katika Mahakama ya Usalama wa Taifa ambayo uamuzi wake hauwezi kukatiwa rufaa.
Sambi ambaye ni mpinzani mkuu wa Rais wa Comoro Azali Assoumani alikuwa tayari amekaa gerezani kwa miaka minne kabla ya kukabiliwa na kesi.