Wednesday , 28th Dec , 2022

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameliomba Kanisa kuelekeza maombi kwa Papa wa zamani Benedict huku akieleza kuwa kiongozi huyo wa zamani ni mgonjwa sana na anahitaji maombi ya dunia nzima

Papa Francis  ameeleza kuwa Benedict XVI amekuwa akipokea matibabu ya mara kwa mara kutokana na afya yake kuzorota 

"Ningependa kuwaomba nyote sala maalum kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict, ambaye analitegemeza Kanisa," Papa Francis ameeleza katika tangazo lake