Tuesday , 10th Jan , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewasema vijana wanaokimbilia utajiri wa haraka badala ya kutengeneza miradi ambayo itaweza kuwaingizia fedha kila wakati.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,

Kauli hiyo ameiotoa hii leo Januari 10, 2023, visiwani Zanzibar, mara baada ya kushiriki kilele cha matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Vijana wa leo tunakimbilia kwenye kutaka utajiri, uwe na jumba zuri, uwe na gari zuri mambo yako yaende hivyo, lakini baada ya muda utajiri ule unakugeuka na kukupiga kama ni jumba zuri huwezi tena kulitunza, unarudi tena kwenye unyonge utajiri ulioutaka kwa haraka haraka unakupiga," amesema Rais Samia

Rais Samia akaongeza "Tunalotakiwa kufanya vijana ni kutengeneza ukwasi, upatikanaji wa fedha kila wakati muwe na miradi midogo midogo, kazi ya serikali ni kufanya makusanyo makubwa na kutekeleza miradi tunayotekeleza, kazi yenu vijana ni kujitengenezea miradi ambayo itawapatieni fedha, fedha ile ndiyo itakayoleta mzunguko,".