
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria inayotarajiwa kuanza Januari 22 mwaka huu jijini Dodoma, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amesema kwa sasa Mahakama inaipa kipaumbele usuluhishi wa migogoro badala ya kufungua mashauri ili kupunguza mzigo kwa mahakama hasa ikizingatiwa usuluhishi umeweza kupunguza asilimia 90 ya mashauri katika nchi zinazoendelea .
Kuhusu wiki ya sheria na siku ya sheria Jaji Mkuu amesema katika wiki hiyo mambo mbalimbali yanayohusu elimu ya sheria yatafanyika mpaka Januari 29 huku siku ya sheria ikitarajiwa kuadhimishwa Februari Mosi ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Katika wiki hiyo ya sheria Mahakama nchini imewataka Watanzania kutumia njia ya utatuzi wa migogoro kwa kutumia usuluhishi ili kuondoa msongamano wa mashauri.