Tuesday , 17th Jan , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashilikia watu 9 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa vifaa vya ujenzi katika mradi wa reli ya kisasa ya SGR pamoja na ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi maarufu kama daraja la JPM.

Daraja la JPM

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema, watu hao wamekamatwa kufuatia operesheni iliyoanza Januari 11, 2023, katika maeneo ya vijiji vya Isunga, Nkalalo, Bukwimba, Malya, na Usagara wilayani Kwimba na Misungwi.

"Katika operesheni hiyo pia tumeweza kukamata mafuta lita 4426, ambapo tumefanikiwa kukamata pia mifuko ya saruji 646 kwa wafanyabiashara tofauti tofauti," amesema Kamanda Mutafungwa

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na pikipiki mali ya Omary Shabani iliyoibiwa Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza yenye namba za usajili MC 450 DLM rangi nyeusi baada ya kuvamiwa na kuporwa katika kijiji cha Mwamanyiri