
Inaarifiwa kwamba katika msimu wa ukeketaji ulioishia mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana zaidi ya watoto 400 walikimbilia katika kituo cha nyumba salama cha ATFGM Masanga lakini baada ya watoto hao kurudishwa nyumbani kwao tayari watoto 70 wamekeketwa
Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee ameagizwa kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria wazazi wa watoto hao 70 waliokeketwa baada ya kurudi nyumbani
Kwa upande wake meneja miradi wa ATFGM Masanga anasema kuwa baada ya msimu kumalizika watoto wanaokimbilia nyumba salama hurejeshwa makwao kwa ajili ya kuendelea na shule lakini kupitia wasiri waliopo vijijini tayari wamebaini uwepo wa watoto hao 70 ambao wamekeketwa licha ya mwaka huu kutokuwa mwaka wa ukeketaji kwa imani za kabila la Kurya
Koo za kabila la kurya huamini mwaka unaogawanyika kwa mbili kuwa ndio mwaka wa Baraka katika masuala ya ukekketaji lakini kipindi hiki imewalazimu kukeketa watoto hao 70 kufuatia kukumbia ukeketaji mwaka jana