
Pichani Jux,Meja Kunta na D Voice
Meja ameshare nyimbo zote katika ukurasa wake wa instagram huku akitupa lawama zote kwa msanii D voice akidai kuwa hakutegemea kama mdogo wake huyo anaweza kumfanyia hivyo licha ya wawili hao kuwa watu wa karibu kuanzia kwa wazazi wao
Kupitia ukurasa wa Instagram Msanii Meja Ameandika...............''D voice Inawezekana Kwenye Hii Game Nikawa Mtu Wa Kwanza Mwenye Ukaribu Nawewe Kutokana Na Ukaribu Wa Familia Zetu.Inawezekana Nikawa Ndie Mtu Niliekufungulia Milango Mingi Kwenye Maisha Yako Tulipofanya Wimbo Wa Pamoja Ulifanya Vizuri Sana
Hii Inaonyesha Kiasi Gani Wewe Ni Mdogo Wangu Wa Rohoni Kabisa Nina Mapenzi Makubwa Na Wewe Ila Hiki Unachofanya Kina Tafsiri Mbili Dharau,Kunitumia, Tunawasiliana Kila siku Tunakutana Kila Siku Sidhani Kama Natakiwa Kulipwa Hiki''