
Mahmoud Hassan - maarufu kama "Trezeguet"
Katika mchezo huo uliochezwa Jumapili usiku kwenye Uwanja wa Hard Rock, Marekani, mabingwa hao wa Misri walitoka suluhu na Inter Miami ya Marekani anayochezea Lionel Messi.
Tukio lililozua gumzo kubwa lilitokea dakika tano kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika, ambapo Al Ahly walipata penalti baada ya Zizo kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Hata hivyo, sintofahamu ilizuka baada ya Trezeguet kuchukua jukumu la kupiga penalti hiyo, licha ya kuwepo kwa mpangilio wa timu unaomtaja mshambuliaji, Wissam Abu Ali kama mpigaji wa kwanza wa penalti.