
Uwanja huo ambao unachukua idadi ya mashabiki zaidi ya 20,500 katika matamasha ya mziki na mashabiki 18,798 kwenye michezo ya mpira wa kikapu pia umezungukwa na hotel na migahawa ya chakula, parking inayochukua Magari 25,000.
Pia ni uwanja wa nyumbani kwa timu ya mpira wa kikapu Minnesota Timberwolves NBA na Minnesota Lynx WNBA ambae atamkaribisha Indiana Fever kutoka ukanda wa Mashariki tarehe 1 Julai.
Kombe hilo limeanzishwa rasmi may 15 2019 na huanza Kila ifikapo tarehe 1 juni mpaka 17 chini ya kamishina wa mpira wa kikapu upande wa wanawake Cathy Engelbert, mpaka sasa baadhi ya timu zilizochukua ubingwa huo ni New York liberty, Settle Storm, Las Vegas Aces na Minnesota lynx bingwa mtetezi alietwaa mwaka 2024 huku Indiana Fever ni mara yake ya kwanza kufika fainali.