Yanga hatuna bahati ya kufunga magoli- Kocha Nabi
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga SC Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kilikosa bahati ya kufunga kwenye michezo mitatu ya Ligi Kuu iliyopita ambayo yote walitoka suluhu. Amesema hayo kuelekea mchezo wao wa Ligi kesho dhidi ya Dodoma Jiji FC utakao chezwa uwanja wa Jamuhuri Saa 10 jioni.