Vijana wakifanya yao katika usahili wa pili wa mashindano ya kudance uliofanyika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jumamosi ya wiki iliyopita.

Baada ya kumaliza usaili wa pili kwa mafanikio makubwa kwa mashindano ya Dance100% 2014 pale viwanja vya Don Bosco Oysterbay,mashindano hayo yatafikia tamati Jumapili hii viwanja vya TCC Chang'ombe katika ngazi ya usaili,kabla ya kuanza kuchuana katika robo fainali,nusu fainali na fainali yenyewe itakayotoa mshindi atakae jishindia pesa Millioni tano.

Mashindano ya Dance 100%2014 ambayo yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania yanazidi kushika kasi na kupokewa vizuri na jamii kutokana na umati mkubwa wa watu ambao huwa unafika katika viwanja husika,kushuhudia michezo mbalimbali pamoja na kujishindia zawadi kemkem zinazotolewa na kampuni ya simu za mikononi Vodacom Tanzania,mbali na zawadi hizo kuna huduma mbalimbali za kimtandao zinazotolewa katika duka maalumu linalokuwepo viwanjani hapo kama kusajiri laini za simu Nk.

Katika usaili wa Jumamosi jumla ya makundi 18 yalijiandikisha na makundi 5 ya makudance yalifanikiwa kushinda,makundi hayo yatashiriki robo fainali na makundi mengine yatakayopatikana siku ya Jumapili katika viwanja vya TTC Chang'ombe na yale 5 mengine yaliyopatikana katika viwanja vya Don Bosco Upanga.katika makundi matano yaliyofanikiwa kupita katika usahili wa pili ni pamoja na Wakali sisi,Pambana Fasaha,Quality boys,Bustani pamoja na Tatanisha Dancers.

Mbali na kucheza kwa uwezo wa hali ya juu vijana wengi walikuwa wakionesha kujipanga kwa mambo mengi kwani waliweza kuonesha utofauti wa mambo mengi ambao uligeuka na kuhamasisha watazamaji na baadae kuamsha shangwe za hali ya juu kwa wale waliokuwa wakifanya vizuri zaidi,pia vijana wengi walijipanga katika suala la muonekano jambo ambalo lilizidi kuonesha kuwa walikuwa wamejipanga kwa kushindana na kuleta mabadiliko katika suala la kucheza kwa sasa.

Katika viwanja vya Don Bosco Osterybay watangazaji mbalimbali wakiwepo wale wa EATV pamoja na East Africa Radio walikuwepo kushuhudia mashindano hayo kama sehemu ya Burudani kwao kutokana na aina mbalimbali ya michezo inayokuwepo katika viwanja hivyo,Akizungumza na EATV mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo Abdallah Khamis 'Dullah' alisema kuwa anajisikia furaha kushuhudia mashindano hayo kutokana na uwezo wa vijana ambao wanakuja kucheza mbele ya majaji ambao ni Lotus Kyamba mtangazaji wa kipindi cha Nirvana,Super Nyamwela na Queen Darlene ambae ni msanii wa Bongo Fleva.

Mbali na zawadi mbalimbali zilizokuwepo katika eneno la tukio pia Kampuni ya TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt, ambacho ndicho kinywaji rasmi kwa ajili ya shindano hilo la Dance 100%2014,walitoa zawadi mbalimbali ambazo zilikuwa zikigombewa na pia kutoa fursa kwa mashabiki waliofika viwanjani kushuhudia michezo mbalimbali ya Baiskeli iliyokuwa ikifanywa na vijana wa Grand Malt.

Shindano la Dance100% 2014 lilifunguliwa na washereheshaji wawili ambao wao ni waigizaji akiwemo Dickson Tegemezi pamoja na Master face muigizaji wa Ze comedy ya EATV,vijana hawa walifungua kwa kuleta radha tofauti viwanjani hapo kabla ya kuwakabidhi Mic washeheshaji maalumu ya shindano hilo ambao ni Tbway 360 (Tony) mtangazji wa kipindi cha 5Seleckt chga EATV na msanii wa muziki aina ya Afro-pop, Menina la Diva.

Mashindano hayo yalifungwa mapema huku kukiwa na ulinzi wa kutosha na viwanjani hapo watu walitawanyika wakiwa salama bila vurugu wala fujo zozote zile baada ya makundi yaliyoshinda kutangazwa na washereheshaji wa Dance100% 2014.

Mpaka sasa makundi 10 tayari yamekwisha patikana ambapo yanaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali ya mashindano hayo likiwepo kundi la The Winners Crew, B2K, TWC, Mazabe Powder,Tam Tam Classic, Wakali Sisi, Pambana Fasaha, Quality Boys, Bustani vilevile Tatanisha Dancers.hivyo bado makundi makundi matano tu ili kuanza kwa robo fainali za mashindano haya.

Katika kwenda kufunga mlango wa usahili wa mashindano haya kabla ya kuanza kwa robo fainali,usahili wa mwisho utafanyika siku ya Jumapili hii katika viwanja vya TTC Chang'ombe hivyo washiriki wakumbe kufika Temeke wakiwa na makundi yasiyopungua watu watano na yasiyozidi watu nane pia wakumbuke kuwa kujiandikisha na kushuhudia mashindano haya ni bure kabisaa na mshindi wa wa kwanza ajajishindia pesa Taslimu million tano.