
Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka shirika la habari la BBC mwanamke huyo bado vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kumtoa baada ya mwanamke huyo kuwasiliana na matabibu akiwa kwenye kifusi.
Mkuu wa kitengo cha kukabiliana na majanga nchini Kenya Pius Masai amesema kwamba wanachora njia ya kuweza kumtoa salama mwanamke huyo.
Aidha idadi ya waliothibitika kupoteza maisha hadi sasa imefikia 33 ambapo watu 80 hadi sasa hawajulikani walipo ambapo juhudi za uokozi bado zinaendelea.