Thursday , 3rd Nov , 2016

Viwango vya riba vinavyotozwa na mabenki pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha nchini Tanzania vitashuka tu iwapo idadi ya watumiaji wa huduma za kibenki wataongezeka na hivyo kuongeza ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha.

Bw. Altemius Millinga

 

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Muungano wa Taasisi za Kifedha unaojulikana kwa kifupi kama TAMFI, Bw. Altemius Millinga, wakati akizungumzia mkutano unaondelea wa wanachama wa mtandao huo, wanajadili mpangilio bora wa shughuli za asasi za kifedha kwenye sheria ya usimamizi wa asasi za kifedha ambayo serikali inakusudia kuja nayo hivi karibuni.

Bw. Millinga amesema idadi ndogo yas watumiaji wa huduma za kifedha zinazotolewa na mabenki ndiyo chanzo cha riba kubwa na kwamba hali inaweza kuwa bora iwapo watumiaji wa huduma za kifedha itaongezeka kama ilivyokuwa kwenye sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi na intaneti.