Kwenye uteuzi huo Rais Magufuli amemteua Mhandisi Alhaji Mussa Ivombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), ambapo kabla ya uteuzi huo Alhaji Mussa Ivombe alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Pia Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Makamo Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi, Prof. Faustine Karani Bee kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF).
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Prof. Tadeo Andrew Satta kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, ambaye awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, kupitia Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.


