Sunday , 20th Nov , 2016

Mtandao wa Asasi za Kiraia zinazotetea marekebisho ya sera na sheria za usalama barabarani ukiongozwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini TAMWA, umeguswa na wimbi la ongezeko la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikigharimu maisha

Bi. Edah Sanga (mwenye gauni la rangi ya pinki)

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi. Edah Sanga ametaja moja ya sababu zinazochangia ongezeko la ajali nchini kuwa ni usimamizi mbovu wa sheria ambazo hata hivyo zimeonekana kuwa na mapungufu yasiyokidhi matakwa ya sasa ya kukabiliana na ajali hizo.

Mmoja wa wanachama wa mtandao huo ni Chama cha Wanasheria Tanganyika – TLS ambapo mwanasheria anayesimamia mradi wa usalama barabarani Bi. Mabesya Rehani amesema wao wakama wanasheria wamekuwa wakitoa msaada wa kisheria kwa idadi kubwa ya wahanga wa ajali wanaokwenda kuomba msaada kwao.

Kwa mujibu wa Bi. Mabesya, TLS imekuwa ikitoa msaada huo kupitia wasaidizi wa kisheria ambao hujulikana kwa kitaalamu kama Paralegal, waliotapakaa maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kutoa msaada kwa makundi ya wananchi wasio na uwezo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Huduma za Kisheria kutoka Chama cha Wanasherkia Wanawake TWLA Bi. Mary Richard amesema wengi wa wahanga wa ajali ni wanawake na watoto kutokana na kundi hilo kupoteza mihimili ya familia zao na kwamba kupitia mfumo huo huo wa paralegal, TWLA imekuwa na dawati maalum la msaada na ushauri wa kisheria ambao hutolewa bure bila malipo yoyote.