Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Seif Shaaban Mohammed
Bw. Mohamed amesema hayo jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kumpongeza rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, kwa kushinda uchaguzi wa marudio ulifanyika machi 20 mwaka huu.
Katibu Mkuu huyo amesema licha ya vitisho vya uvunjifu vya amani vilivyokuwepo lakini suala hilo halikutokea kutokana na kuimarika kwa ulizn ina usalama visiwani humo ulisimamiwa na vikosi vya Ulinzi vya Zanzibar na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Aidha Bw, Mohammed amesisitiza ulinzi huo uliokuwepo kabla ya uchaguzi na baada ya Uchaguzi Uendelee kwa kuwa mwisho wa Uchaguzi wa kwanza ndio mwanzo wa Uchaguzi wa pili na kusema kuwa kwa kuwa uchaguzi umekwisha si vyema Zanzibari ikaachwa bila ulinzi uliokuwepo tangu awali.
Aidha amewapongeza Wanzanzibar kwa kupiga kura kwa usalama na amani na kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka kwa ngazi zote ikiwemo ya Urais na Wawakilishi.