
Akizindua kampeni hizo, Dk. Nchemba amewataka wananchi wa jimbo la Longido kumchagua mgombea wa CCM, Dk. Steven Kiruswa awe mbunge wao kutekeleza ilani ya chama mapinduzi kwa kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.
Dk. Mwigulu amesema wapinzani wameogopa kuwa wataachwa mbali katika baada ya kupima uitikio wa wananchi ambao wanakubali kazi za Rais John Magufuli na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na wananchi wanaona.
Aidha Dk. Mwigulu amewahakikishia wananchi wajitokeze siku ya kupiga kura kwani usalama ni wa uhakika wakati wa kupiga kura.