Thursday , 29th Nov , 2018

Msanii mkongwe wa Hip-hop nchini, Ambwene Yessayah (A.Y) amefunguka kuwa kwa sasa hawezi sema ni lini ataachana na muziki mpaka pale muda utaporuhusu yeye kufanya hivyo.

AY akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, ambapo alikuwa akitambulisha wimbo wake wa 'SAFARI' alioufanya na King Kikii, AY amesema kuwa bado ana nyimbo nyingi amezihifadhi na hawezi kuacha zipotelee ndani.

"Sijafikiria bado kuacha muziki bado stock imejaa, ngoja tuone muda ukifika ila kwa sasa ngoja niachie ngoma kwanza", amesema AY.

Aidha ameongeza kuwa hali ya muziki wa kizazi kipya nchini, inaridhisha na kuzidi kuwapa moyo wa kupambana wasanii kupitia changamoto za kimaendeleo.

"Ninapoona muziki unachangamka ndio furaha yangu, kwakweli mimi napenda sana ligi, hilo hata watu wa karibu yangu wanajua naweza kukaa na watu kumi nikawatuliza wote", amesema AY.