
Nay wa Mitego
Akizungumza katika Friday Night Live (FNL) ya EATV, Nay amesema kuwa mwanzo alikuwa naonesha magari, nyumba, na biashara zake kwasababu mama yake hakuwa akijua, lakini alipokuja kugundua alimpiga 'Stop'.
"Mimi nimeacha hivyo vitu, huwa namsikiliza sana bi mkubwa wangu (mama), alikuwa hajuagi mambo ya mitandaoni lakini ilifika 'time' kuna mtu akaenda kumuonesha baadhi ya vitu akaniambia "no mimi sipendi hivi", amesema Nay.
"Kama una kitu na unataka kuoneakana basi kawatolee watu", ameongeza Nay.
Nay ameachia wimbo wake mpya wiki hii unaojulikana kwa jina la "Mbele kwa mbele", na unaonekana kupokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wake.
Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.