Wednesday , 16th Jan , 2019

Moja ya matukio makubwa kwenye soka duniani ni uhamisho wa Cristiano Ronaldo ambao kwa namna moja ama nyingine umeacha athari kubwa kwa mashabiki wa Manchester United.

Mabadiliko hayo katika picha.

Miaka 10 iliyopita nyota huyo raia wa Ureno alikuwa akiichezea Manchester United hadi Julai 1, 2009 ambapo rasmi alijiunga na Real Madrid na kusababisha baadhi ya mashabiki wa Man United kuhamia Real Madrid kumfuata mchezaji huyo.

Ilikuwa ni msimu mmoja tu umepita wa 2007/08 ambapo klabu hiyo ilikuwa imeshinda ubingwa wa Ulaya ambao mpaka sasa haijawahi kushinda.

Ronaldo pia aliibuka mchezaji bora wa dunia mwaka 2008 ambapo tangu hapo hakuna mchezaji anayecheza Ligi Kuu ya Uingereza EPL ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.

Pia Ronaldo alikuwa ndio mchezaji aliyekuwa amefunga mabao mengi katika msimu mmoja wa EPL (31) rekodi ambayo ilifikiwa na Luis Suarez msimu wa 2013/14 kabla ya kuvunjwa na Mohamed Salah msimu uliopita kwa kufunga mabao 32.

Miaka 10 imemalizika kwa historia nyingine baada ya baadhi ya mashabiki wa Man United kulazimika kuanza maisha mapya kwa kuifutilia Juventus baada ya nyota huyo kutua huko akitokea Real Madrid mnamo Julai 10, 2018.

Katika miaka 10 aliyokaa Real Madrid Ronaldo amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 450.