
MSerbia huyo mwenye umri wa miaka 28 alithibitisha udedea wake alipomlamza Murray seti tatu kwa nunge za alama 6-1 7-5 7-6 (7-3) huko Melbourne Park.
Kichapo hicho ni cha 5 kwa muingereza Murray ambaye sasa ameshindwa katika fainali zote 5 alizowahi kushiriki za mchuano wa wazi wa Australia,na 4 kati ya hizo akipoteza kwa Djokovic.
Murray mwenye umri wa miaka 28,sasa ameingia katika kumbukumbu kwa kushindwa katika fainali 5 za Grand Slam za tenis tangu kuasisiwa kwa mashindano hayo ya wazi mwaka wa 1968.
Kwa upande wake Djokovic alisajili ushindi wake wa 6 mjini Melbourne na sasa anatoshana nguvu na bingwa wa zamani Roy Emerson kutoka Australia.
Djokovic vilevile ametoshana makali na vigogo wa mchezo huo Bjorn Borg na Rod Laver waliowahi kushinda mataji 11 ya Grand Slam.