Friday , 6th Mar , 2015

Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA kimesema kutokana na mpangilio wa ratiba ya michuano ya klabu Bingwa Mkoa wa Dar es salaam iliyapangwa kufanyika kila mwishoni mwa wiki imeahirishwa kwa wiki hii.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa DAREVA, Siraju Mwasha amesema, michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Februari 28 mwaka huu kwa kushirikisha vilabu saba vya wanaume na vilabu saba vya wanawake kutoka mkoa wa Dar es salaam imekuwa na changamoto nyingi kutokana na vilabu shiriki kuwa na muda mrefu wa kujiandaa na michuano hiyo.

Mwasdha amesema, vilabu hivyo vimekuwa vikijiandaa kwa muda mrefu kabla ya kuanza mashindano hayo ambapo baada ya kuanza michuano hiyo pia vinapata muda mrefu wa kujiandaa kwani katika wiki wanakuwa na siku tano za kujiandaa.

Mwasha amesema, ushindani umeongezeka kutokana na baadhi ya timu shiriki za mkichuano hiyo kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na baadhi ya timu zimekaa muda mrefu bila kushiriki michuano ya aina yoyote.