
Mchezo huo utaanza majira ya saa 10:00 mchana huku macho ya mashabiki wa Simba yakiwa yanaelekezwa kwa klabu hiyo kwa kuwa na kiu ya kushinda mchezo wao wa kwanza.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana huku Singida United wakitolewa na wapinzani wao AFC Leopards kwa matuta baada ya kutoa sare ya 1-1 mpaka dakika 90 za mchezo kuisha.
Huku nao mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwachakaza Tusker FC ya kenya kwa mikwaju ya penati baada ya kumalizika mchezo bila ya kufungana.
Bingwa wa michuano hii atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 30,000 (zaidi ya Sh. Milioni 65) za Tanzania pamoja na nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Everton ya England.
Kabla ya mchezo wa Simba kuanza hapo saa 10 jioni, mchezo kati ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya watapelekeshana majira ya saa 8 :00 mchana kutoka katika viwanja hivyo hivyo.