Saturday , 18th Jan , 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bashiru Ally amesema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, katika kiti cha Ubunge na Halmashauri ya Kigoma Mjini, ambayo inaongozwa na Mbunge Zitto Kabwe, na Chama Cha ACT - Wazalendo.

Bashiru Ally ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wake na wanachama wa chama hicho Kigoma Mjini, ambapo amesema wapinzani wao wajiandae kushindwa.

Bashiru amesema kuwa "CCM tukishindwa tukubali tumeshindwa, tuliposhindwa Kigoma Mjini tulikubali, na wajifunze kuwa aliyeshindwa akirudi awamu ya pili akakung'oa na yeye akubali"

"Niwaambie Kigoma Mjini na Kigoma nzima ambapo hatukushinda, tumejipanga kushinda, wajiandae kushindwa" amesema Bashiru