
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, leo Agosti 24, 2021, Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini SACP David Misime amesema kuwa, kufunguliwa kwa kikao kazi hicho na Mhe. Rais kutatoa fursa kwa Makamanda hao kufanya tathimini ya utendaji kazi kuona mafanikio na changamoto na kutokana na mikakati mbalimbali ya kutekeleza jukumu lake kuu la kulinda maisha ya watu na mali zao.
Aidha, Msemaji wa Jeshi hilo ameongeza kuwa, katika kikao kazi hicho pamoja na watoa mada wa ndani ya Jeshi hilo pia utahusisha wadau mbalimbali wa kiraia kama sehemu ya watoa mada mbalimbali zilizoandaliwa.
Tazama Video hapo chini