Monday , 30th May , 2022

Polisi Mkoani Mwanza wamethibitisha kuwa Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mke wake Swalha Salum naye  amejiua kwa kujipiga risasi na mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amesema Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani na ndugu zake wameutambua mwili huo kuwa ni wa ndugu yao