
Barre ametoa maelezo hayo kwenye televisheni ya taifa la nchi hiyo baada ya vikosi vya usalama kumaliza mapambano dhidi ya vikosi vya al-Shabab ambayo yalidumu kwa saa 35 kwenye hoteli hiyo maarufu
Waziri huyo mkuu ameongeza kwamba tukio hilo halikubaliki na kwamba kila afisa usalama ambaye hakutimiza majukumu yake ni lazima awajibike
Waziri wa afya nchini humo Ali Hajji Aden amesema kuwa takribani watu 21 wameuawa kwenye mapambani hayo huku wengine 117 wakijeruhiwa
Waziri mkuu huyo alifanya ziara ya kuwatembelea waliohjeruhiwa na kwamba walio kwenye hali mbaya zaidi watapelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi
Shambuzli i hilo lililofanywa wiki iliyopita huku lilitibitishwa na tovuti al shabab, limepelekea wananchi kuikosoa serikali kwa kushindwa kumaliza mara moja mapambano hayo yaliyogharimu maisha ya watu