Tuesday , 4th Oct , 2022

Korea Kaskazini imerusha makombora makali yaliyovuka anga la Japan kwa kile kilnachoonekana kwamba ni kutaka kusikia Tokyo na Japan zitasema nini juu ya jaribio hilo.

 Kombora hilo limesafiri umbali wa kilomita  4,500 sawa na maili 2,800 na kisha kuanguka katika bahari ya Pacific .

Hili ni jaribio la kwanza la Korea Kaskazini kurusha kombora kuelekea Japan tangu mwaka 2017.  Japan imewataka wananchi wake kuchukua tahadhari huku Marekani na Korea Kusini zikijibu mapigo.

Mkuu wa kikosi cha anga wa Korea Kaskazini amesema kwamba makombora manne yamefanyiwa majaribio katika mazoezi ya kawaida.Amesema mazoezi hayo yalilenga maeneo ambayo hayakaliwi na binadamu .  Umoja wa mataifa umeizuia Korea Kaskazini kufanya majaribio hayo ya nyuklia  huku ilijulikana kwamba kurusha makombora bila ridhaa ya nchi nyingine ni kosa la kimataifa.