
Wakizungumza na EATV wakazi hao wamesema kuwa tatizo hilo linasababisha taka kuzagaa hovyo na kwamba asilimia kubwa ya wanaofanya vitendo hivyo wanafanya makusudi, maana ni maeneo machache ambayo hayana sehemu za kukusanyia taka
Wakizungumzia tatizo hilo wenyeviti wa mitaa ya Buyekera Asili na Mtoni wamewataka wananchi kuacha tabia hiyo mara moja na badala yake watumie maeneo yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutupa taka, huku diwani wa kata Bakoba, Shaban Rashid akidai wakaobainika kuendelea na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za halmashauri