
Bendera ya CHADEMA
Akizungumza na EATV&Radio Digital, Mrema amesema kuwa, Bunge hilo lina nia ya kuwasilisha kero za wananchi kwenye serikali kuu na zipatiwe ufumbuzi, kwa madai ya kwamba wabunge waliopo bungeni hawafanyi jambo hilo.
"Wajumbe wa Bunge hili ni wale wagombea wa CHADEMA waliogombea katika majimbo katika uchaguzi mkuu uliopita, litakuwa linatoa maoni mbadala na kuishauri serikali kwenye mambo yote na litawafikia wananchi, na kero zote zitakusanywa na kuwasilishwa serikalini kwa njia mbalimbali," amesema Mrema