
Mtoto aliyetaka kunyongwa
Majirani wa mtaa huo wamesema mama huyo amekuwa na kawaida ya kumpiga mara kwa mara mtoto pindi anapokosea na kumsababishia majeraha kwenye mwili wake hadi hapo juzi alipoamua kumpiga vibaya na kumnyonga huku akiwa amefungulia redio kwa sauti ya juu ili asisikie mtu yoyote.
Hamisa Juma ni mtoto wa mama huyo anaeleza tukio lilivyokuwa wakati mdogo wake akinyongwa
"Alikuwa amesimama kwenye hii nyumba ya kwanza, alivyomuona amesimama akamuita na kuanza kumpiga Love na mwiko, mama ndiye alikuwa anampiga akampiga sana baadae nikamwambia Love kimbia uende nje akawa anampiga tu hadi baadae akanyonga," ameeleza mtoto huyo
Musa Fereji mwenyekiti wa mtaa wa Mission anaeleza hatua alizochukua baada ya kupata taarifa za mtoto kunyongwa
"Nilipigiwa simu na wananchi kwamba kuna mama mmoja kwamba alikuwa ananyonga mtoto kweli hicho kitendo kilinishtua sana ikabidi niwatafute wajumbe wangu tukaenda tukamkuta huyo mama akiwa ndani tukamkamata na huyo mtoto kweli alikuwa anaonyesha dalili za kunyongwa maana alikuwa amekabwa shingoni na koromeo,"