Thursday , 12th Jan , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia Mapinduzi Siliya (45), mkazi wa Nzovwe, kwa tuhuma za kumuua mke wake Terezia Mtajiha, kwa kumchinja na kisu shingoni kisha kwenda kuutupa mwili wake Mto Nzovwe, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Aliyemuua mke wake akiwa mikononi mwa polisi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP, Benjamin Kuzaga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea Januari 11 mwaka huu majira ya  saa 7:00 mchana eneo la Nzovwe jijini humo na kueleza chanzo cha mauaji hayo.

"Alimuua mke wake kwa kumchinja na mwili wake kwenda kuutupa mtoni, kisa cha mauaji haya ni kumtuhumu mke wake kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine," ameeleza ACP Kuzaga