Monday , 16th Jan , 2023

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameagiza walimu kuwapokea wanafunzi  wanaojiunga na kidato cha kwanza hata kama hawajakamilisha mahitaji baada ya kubainika kuwa kati wanafunzi 14,904 waliofaulu ni wanafunzi 3,779 sawa 25 % pekee ndio walioripoti kuanza kidato cha kwanza

Takwimu hizo zimetolewa na Katibu tawala Mkoa Hassan Rugwa katika kikao kazi cha tathmini ya mwendo wa elimu.
Imeelezwa kuwa mkoa wa Katavi kwa upande wa elimu msingi unakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa zaidi ya 3800 Hali inayopelekea baadhi ya shule kukaa wanafunzi zaidi ya 200 kwa darasa Moja.

Nao baadhi ya waalimu wamesema utoro unatokana na shule kuwa mbali na makazi na msongamano wa wanafunzi darasani pia unasababisha ufaulu kushuka hasa kwenye mitihani ya kitaifa.