Dkt. Mollel amesema hayo leo Februari 09, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Stella Manyanya katika Mkutano wa kumi kikao cha nane, Bungeni Jijini Dodoma.
“ Katika kuboresha hospitali ya Rufaa ya kanda ya kusini, tayari Serikali imetoa jumla ya shilingi Bilioni 4.4 itayosaidia kujenga majengo ya nyumba za wafanyakazi, ujenzi wa chumba cha kuhufadhia maiti, umaliziaji wa maabara na umaliziaji wa jengo la mama na motto”
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Serikali inaendelea kuboresha huduma nchini, na tayari Serikali imeanza kupeleka madaktari bingwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kusini, huku vifaa kama CT-SCAN pamoja na MRI vikiwa tayari vimefungwa tayari kuanza kutoa huduma


