Tuesday , 28th Mar , 2023

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuingiza nchini boksi 1052 za vipodozi vyenye viambata vya sumu kutoka nchi jirani ya Zambia kwa kutumia lori la kusafirisha mafuta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa eneo la Kijiji cha Songwe, Kata ya  Bonde la Songwe wilayani Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri na kuweka mtego uliofanikisha kuwatia mbaroni.

Nae Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Mkoa wa Mbeya,  Musibu Shaban amesema bidhaa zilizokamatwa ni za magendo na kwamba taratibu za kisheria zitafuatwa.