''Wahanga Karume watafutiwe eneo'' - RC Makalla
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla,amewaomba wahanga wa moto Soko la Karume kuwa watulivu, kwani inaundwa kamati ya kuchunguza chanzo cha moto katika Soko la Karume ambapo vyombo vyote ya ulinzi na usalama pamoja na Afisa Biashara Jiji na mkoa wataingia kwenye kamati hiyo.