Kamati ya pili ya mchanga yapangiwa majukumu
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Aprili, 2017 amewaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria itakayochunguza mchanga wenye madini ulio katika makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini.