Majaliwa afanya haya kabla ya Magufuli kuapishwa

Jumatano , 4th Nov , 2020

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa leo Novemba 4, 2020, ameongoza viongozi wakuu wa serikali, kukagua uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wengine wa serikali

Uwanja huo ndipo kutafanyika shughuli ya kuapishwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho, Novemba 5, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, amesema maandalizi yamekamilika na matarajio ni kupokea wageni zaidi ya thelathini kutoka nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na marais wa nchi mbalimbali na mabalozi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge na Kamanda wa polisi Dodoma Gilles Muroto, kwa pamoja wamesema ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kiwango cha hali ya juu na kutoa wito kwa wananchi kuhudhuria kwa wingi tukio hilo la kihistoria.