Chama: 
ADA-TADEA
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Hassan Kornely Kijogo
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Mgombea Ubunge Maswa Magharibi (ADA TADEA), hakushinda
Idadi Ya kura: 
33 086

Alizaliwa Februari 23, 1950, katika Hospitali ya Ndanda Masasi mkoani Mtwara.

Mwaka 1959 alisoma Shule ya Msingi Sayusayu, Maswa. Mwaka 1962 alihitimu darasa la nne. Mwaka 1963, alichaguliwa kuendelea na darasa la tano katika Shule ya Seminari ya Makoko iliyoko Musoma mkoani Mara.

Mwaka 1966, Shibuda alihitimu darasa la nane na 1967 alijiunga na masomo ya sekondari, shule ya ufundi Moshi. Mwaka 1970 alihitimu Cheti cha Uhandisi wa Mitambo na 1971, aliajiriwa na kampuni ya kimataifa ya matairi duniani ya General Tyre International ya Marekani.

Akiwa kazini hapo, alipewa ofa ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Akron, Ohio kusomea Shahada ya Uhandisi wa utengenezaji matairi. Mwaka 1973, Shibuda alitunukiwa Shahada ya Uhandisi wa uzalishaji wa matairi.