Chama: 
UPDP
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Ramadhan Ali Abdallah
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
6 184

Alizaliwa Februari 14, 1952 katika Kijiji cha Kiwawa Kigongo, kilichopo Kilwa Masoko mkoani Lindi.

Mwaka 1963, alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Lihimalyao, wilayani Kilwa na alihitimu darasa la nne mwaka 1964.

Mwaka 1965 alichaguliwa kuendelea na darasa la tano katika Shule ya Msingi Msanga iliyopo Kilwa Masoko na alisoma hadi darasa la sita mwaka 1966 kabla ya kuhamia Shule ya Msingi Pande-Extended alikomaliza darasa la sita na kuhitimu darasa la saba mwaka 1967.

Mwaka 1970, aliajiriwa na kiwanda cha nguo cha Urafiki na baadaye mwaka 1984 alipewa nafasi kujiendeleza kwa masomo ya sekondari.

Mwaka 1988 alifanya mtihani wa kidato cha nne kama mtahiniwa binafsi. Mwaka 1989 alisoma Astashahada ya teknolojia ya utengenezaji nguo.

Mwaka 1998 aliendelea tena na masomo ya kidato cha tano, ingawa hakumaliza kidato cha sita baada ya utaratibu huo kuondolewa Urafiki.