Chama: 
NCCR MAGEUZI
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Khamis Haji Ambar
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
19 696

Alizaliwa Desemba 24, 1967. Mwaka 1974 alianza elimu ya msingi na kuhitimu darasa la saba mwaka 1980 katika Shule ya Msingi Balili mkoani Mara.

Mwaka 1983 alijiunga na kidato cha kwanza Shule ya Sekeondari ya Ilboru, Arusha na mwaka 1987 alijiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Tosamaganga, Iringa na kuhitimu kidato cha sita mwaka 1989.

Maganja alijiunga na mafunzo ya kijeshi ya mwaka mmoja (1989 mpaka 1990).

Mwaka 2005 alidahiliwa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam alikosoma Shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Biashara na kuhitimu mwaka 2008. Mwaka 2009 alidahiliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro kwa Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara na kuhitimu 2011. Pia alisoma Stashahada ya masomo ya Kompyuta.