Chama: 
AFP
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Rashid Ligania Rai
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
4 635

Wasifu wake unaanza Januari 20, 1974 alipozaliwa huko Vikokoteni, Wilaya ya Mjini Zanzibar.

Alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Zanaki, Dar es Salaam, mwaka 1984 na kuhitimu 1990. Mwaka 1991 alijiunga na Sekondari ya Forodhani, Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1994.

Mwaka 1995 hadi 1997, alijiunga na Shule ya Kiislamu ya Alhraiman, Dar es Salaam na mwaka 1998, alisoma astashahada ya Uandishi wa Habari na Uhusiano wa Kimataifa kwenye Kituo cha Mafunzo ya Uandishi wa Habari Televisheni ya Zanzibar (TVZ).

Mwaka 2000, alijiunga na Chuo Kikuu cha Clarke, kilichopo Boston, Massachusetts, Marekani alikosoma Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta na kuhitimu 2004.