Chama: 
CUF
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Hamida Huweishil Abdalla
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
72 885

Prof. Ibrahim Lipumba (CUF)

Alizaliwa Juni 6, 1952 mkoani Tabora. Mwaka 1959 alianza Shule ya Msingi na mwaka 1977 alichaguliwa kujiunga Sekondari ya wavulana Tabora.

Alianza elimu ya msingi 1959 - 1962 katika Shule ya Msingi ya Swedish Free Mission Primary School, Sikonge 1962 - 1966: L.A Upper Primary School, Sikonge na baadaye kuendelea masomo na elimu ya Sekondari 1967 hadi 1970 katika Sekondari ya Wavulana Tabora, na 1971 hadi 1972 Pugu Sekondari kidato cha tano na sita. Kisha Elimu ya Chuo Kikuu mwaka 1973 hadi 1977 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alihitimu Shahada ya Uchumi pamoja na Shahada ya Uzamili ya Uchumi.

Mwaka 1978 hadi 1983 alijiunga Chuo Kikuu cha Stanford University nchini Marekani kwa masomo ya uzamivu.

Profesa Lipumba anagombea urais wa Tanzania mara ya tano sasa.