Chama: 
ADC
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Khamis Juma Shoka
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Mgombea Ubunge Kawe (ADC), hakushinda
Idadi Ya kura: 
7 627

Alizaliwa Juni 4, 1974 na Januari 1982, Queen akiwa na miaka saba aliandikishwa kuanza darasa la kwanza Shule ya Msingi Mapambano na alihitimu mwaka 1988.

Mwaka 1989, alijiunga na Shule ya Sekondari Shighatini iliyopo Mwanga, Kilimanjaro na kuhitimu mwaka 1992. Mwaka 1994 alijiunga na Chuo cha Msimbazi Center, Ilala Dar es Salaam kwa ajili ya Astashahada ya Ualimu wa watoto na alihitimu mwaka 1996.

Mwaka 2007, Queen alijiunga na Chuo cha Global kilichopo Dar es Salaam kwa mwaka mmoja na kutunukiwa Astashahada ya Masoko na Mauzo. Pia alisoma kozi nyingi fupi fupi za masuala ya biashara.

Mwaka 2008, alidahiliwa na Chuo Kikuu (SAUT), akisomea shahada ya Usimamizi wa Biashara hadi mwaka 2011 alihitimu shahada yake.