Chama: 
CHAUMA
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Mohammed Massoud Rashid
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Mgombea Urais (Kura 49,256), hakushinda
Idadi Ya kura: 
32 878

Hashim Rungwe (CHAUMMA)

Alizaliwa Januari 1, 1949 katika mji mkongwe wa Ujiji, Kigoma. Alianza Shule ya Msingi Kipamba iliyopo Ujiji na kuhitimu darasa la nane mwaka 1966. Mwaka 1967 alisoma masomo ya Sekondari kupitia Taasisi ya Cambridge, kisha alifanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 1969 kama mtahiniwa binafsi. Kati ya mwaka 1975 hadi 1991 alipitia mafunzo mbalimbali na kutunukiwa Stashahada kadhaa.

Mwaka 1996, Rungwe alidahiliwa Chuo Kikuu Huria kusoma Shahada ya kwanza ya sheria na alihitimu mwaka 2004. Mwishoni mwa miaka 1970, Rungwe aliwahi kufanya kazi ya umma, kabla ya kugeuka biashara na anawania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya tatu sasa.