Chama: 
UMD
Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais): 
Mashavu Alawi Haji
Matokeo ya Uchaguzi 2015: 
Hakushiriki uchaguzi
Idadi Ya kura: 
3 721

Khalfan Mohamed Mazrui (UMD)

Amezaliwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Mwaka 1983, alianza darasa la kwanza na ilipofika mwaka 1987 akiwa darasa la tano alikatisha masomo baada ya wazazi wake kuhamisha makazi.

Maisha ya kielimu hayakuwa upendeleo kwake kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo wa kumsomesha zaidi. Hivyo aliamua kujiendeleza hadi sekondari. Alijiunga na Taasisi ya Elimu ya Watu wazima, akawa anasoma kituo cha Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.

Mwaka 2005, alifanya mitihani ya kidato cha pili katika kituo cha Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Ilala Dar es Salaam. Japokuwa Mazrui anasema alipata ufaulu mzuri, kutokana na changamoto za kimaisha, alishindwa kuendelea zaidi na masomo.